Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kwa furaha na bashasha kubwa, wakazi wa Jiji la Tanga wamewapokea wageni maalumu – Timu ya Wasomaji wa Qur'an Tukufu toka Nchini Iran, wanaobobea katika usomaji wa Tajweed. Ujio wao ni sehemu ya maandalizi ya tukio kubwa la Kiislamu na la Qur'an Tukufu, linalotarajiwa kufanyika jijini humo Siku ya Jumamosi.
Kesho, Jumamosi, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana, Kongamano Kubwa la Qur'an Tukufu litafanyika katika Uwanja wa Mkwakwani, likihusisha usomaji wa Qur'an kwa ladha na sauti za kuvutia, kwa kufuata kanuni sahihi za Tajweed.
Wenyeji wa Tanga, viunga vyake, na wageni kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania mnakaribishwa kwa wingi kuhudhuria na kushiriki katika kongamano hili la kiroho.
Njooni tusikilize maneno matukufu ya Mwenyezi Mungu, yanayoteremsha utulivu moyoni na kuongoza katika njia ang’avu ya haki na uongofu.
"Hakika hii Qur'an ni muongozo bora na ni ponyo kwa nyoyo za waja wa Mwenyezi Mungu."
Your Comment